kesha la asubuhi
KESHA LA ASUBUHI
JUMAMOSI, DESEMBA, 26, 2020
SOMO: KUABUDU PAMOJA
Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, mtakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Na itakuwa, mwezi mpya hata nwezi mpya, na sabato hata sabato wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.
Isaya 66:22, 23
Hapo mwanzo Mungu Baba na Mwana walipumzika katika siku ya Sabato baada ya kazi yao ya uumbaji. Wakati ambapo mbingu na nchi zilikuwa zimemalizika, na jeshi lake lote, Muumbaji na viumbe wote wa mbinguni walisherehekea kwa kutafakari juu ya mwonekano wa utukufu. "Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, na wana wote wa Mungu walipopiga kelele za furaha."
Wakati wa "kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu," Sabato ya Uumbaji, siku ambayo Yesu alipumzika katika kaburi la Yusufu, itadumu kuwa siku ya pumziko na kufurahia. Mbingu na dunia zitaungana katika kusifu, Itakuwa sabato hata sabato mataifa ya waliokombolewa watasujudu katika ibada ya furaha kwa Mungu na Mwanakondoo.
Mataifa ya waliokombolewa hawatafahamu sheria nyingine yoyote isipokuwa sheria ya mbinguni. Wote watakuwa wenye furaha, walioungana, wakiwa wamevikwa mavazi ya sifa na shukrani. Katika mandhari hiyo nyota za asubuhi zitaimba pamoja, na wana wa Mungu watapiga kelele za furaha....
"Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana." "Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, Na wote wenye mwili watauona pamoja." Bwana Mungu ataotesha haki na sifa mbele ya mataifa yote. Katika siku ile Bwana wa majeshi atakuwa na taji ya fahari, na kilemba cha uzuri, kwa mabaki ya watu wake.
Kama vile ambavyo mbingu na nchi zitakuwepo milele, Sabato itadumu kuwa ishara ya nguvu za Muumbaji. Bustani ya Edeni itakapostawi kwa mara nyingine hapa duniani, siku takatifu ya Mungu ya kupumzika itaheshimiwa na wote
Post a Comment