Kufanikiwa kama Mkristo ipo hivi
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA ILI MKRISTO AWEZE KUFANIKIWA. ( Sehemu A )
BY. MWALIMU DALALI DAVID MARCO
Tunamfahamu tajiri wa nyakati zote kati ya wanadamu. Nabii Sulemani, aliyepata kibali machoni pa Mungu licha ya dhambi alizowahi kutenda.
Alipewa fursa ya kuomba neno lolote 1Fal 3:5....Hebu fikiria ungekuwa ni wewe ungeomba kitu gani?
Sulemani akaomba apewe hekima na akili nyingi. 1Fal 3:9,11
Mungu akampa Sulemani akili nyingi kupita watu wote baada na kabla yake.
Je, waweza kufikiria kuwa Sulemani alikuwa na akili namna gani? 1Fal 3:12 ; 1Fal 4:29
Kwa kuwa ombi la Sulemani lilipata kibali, Mungu akampa hata na vile ambavyo hakuviomba 1Fal 3:15
TUNU ZA SULEMANI
- Alinena mifano 3000
- Aliimba nyimbo 1005
- Kwa siku moja familia yake iliweza kuandaa mlo wa viwango.
+ kori 30 za unga wa kawaida mzuri
+ kori 30 za unga wa ngano
+ ng'ombe 10 walionona
+ kondoo 100
+ ayala walionona
+ paa walionona
+ kulungu walionona
+ kuku walionona
1Fal 4:22-23
Mbali na hivyo Sulemani alikuwa mwalimu smart sana katika shule ya elimu ya mimea, wanyama, ndege na vitambaavyo na samaki.
( Bila shaka kwa utaalamu wake nabii, COVID-19 Isingegusa familia yake )
1Fal 4:33
Kwa hekima kubwa aliyokuwa nayo alisikilizwa na watu tena hata wakuu na marais wa nchi mbalimbali duniani kote.
1Fal 4:34
Mungu alimpa amani kila upande 1Fal 5:4
Kwa shukrani kubwa nabii alimjengea Mungu hekalu kwa miaka saba
1Fal 6
Mpendwa hebu tufikirie maisha yetu tunamtambulishaje huyu Mungu kwa watu wengine...je, liko jambo jema tulilowahi kutenda lipasalo baraka iletayo rehema kwa dhambi zetu? Wapo wahitaji kila mahali je, umewahi kufikiria kupeleka sadaka yako sehemu tofauti na kanisani? Mara nyingi sadaka itolewayo kanisani imelekuwa ni ya mashindano....unapita mbele kuweka sadaka yako ili uonekane kuwa unamcha Mungu...unapitia lesoni na Biblia pamoja na kesha kwa kurukaruka ili umalize upate wasaa wa kunyosha mkono kwa darasa la shule ya Sabato...
Umewahi kufikiri kwa kina umuhimu wa taarifa za utume?
Tusienende kwa mazoea, kununua lesoni haikuonyeshi kuwa wewe ni mcha Mungu sana.. God needs your kindness....
Siku ile ya mwisho wapo watu tuliowatazama kwa wingi wa dhambi zao tutawashuhudia wakiuingia mji na kushangaa sisi tukibaki nyuma na marafiki zetu tuliopatana nao kama wasafi kanisani.
Ifikie mahali kanisa lirudi katika misingi yake ...tuipiganie haki ya Mungu wetu ili watu wajue njia ya kweli.
MPENDWA NAKUSIHI TUTAFAKARI MIENENDO YETU KAMA INAWAVUTA WENGINE KWA KRISTO.
MUNGU ATUHURUMIE.
Post a Comment