amka na Bwana

KESHA LA ASUBUHI

Jumatano 30/12/2020

*SABABU ZA PAMBANO KUU KURUHUSIWA*

*Na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; ili sasa kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo na namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho.* Waefeso 3:9,10

📜 Kwa nini pambano kuu liliruhusiwa kuendelea katika zama zote? Kwanini uwepo wa Shetani haukuondolewa mara tu alipoasi? —ilikuwa ni ili ulimwengu uweze kutambua haki ya Mungu katika kushughulika kwake na uovu, ili dhambi ihukumiwe milele. Katika mpango wa ukombozi kuna marefu na mapana ambayo umilele pekee hautoshi kuyaeleza, maajabu ambayo malaika wanatamani kuyaona.

📜 Waliokombolewa pekee, katika viumbe vyote vilivyoumbwa, watakuwa wamefahamu pambano dhahiri la dhambi katika uzoefu wao wa maisha; wametendakazi na Yesu, na wameingia katika ushirika wa mateso yake kiasi ambacho hata malaika hawakuweza kufanya hivyo... Naye "akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika Ulimwengu wa roho: ...ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu."

📜 Kadri mataifa ya waliookolewa watakavyomtazama Mkombozi, na kuuona utukufu wa milele wa baba ung'aao katika sura yake; watakapokuwa wakikitazama kiti cha enzi, ambacho kitakuwepo milele hata milele, na kufahamu kuwa ufalme wake hautakuwa na mwisho, watainuka kuimba wimbo wa furaha kuu...

📜 Rehema, huruma, na upendo wa Baba unaonekana ukiwa na utukufu, haki, na nguvu. Tunapokuwa tukikitazama ukuu wa kiti cha enzi, kilichoinuliwa juu, tutaiona tabia yake kupitia neema yake aliyotupa, na kuifahamu, kuliko ilivyokuwa hapo awali, maana halisi ya jina la kupendeza la Baba Yetu.

🔘 *Matokeo ya pambano kati ya Mwokozi na nguvu za giza yatakuwa ni furaha kwa waliokombolewa, ikichangia kwa utukufu wa Mungu milele zote.*

*TAFAKARI NJEMA SANA*👮‍♂️

No comments