KILO 242 ZA DAWA ZA KULEVYA ZATEKETEZWA MOTO

KILO 242 ZA DAWA  ZA KULEVYA  ZATEKETEZWA

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya (DCEA) leo imeteketeza jumla ya kilo 242 za dawa za kulevya aina ya Heroine, Cocaine na bangi, ambazo kesi zake zimetolewa hukumu na Mahakama Kuu"

Idadi ya dawa hizo ilikuwa ni Heroine kilo 119, Cocaine kilo 3 na bangi kilo 120 zilizotokana na kesi mbalimbali zilizotolewa hukumu kuanzia mwishoni mwa mwaka jana"

Kazi hiyo ilishuhudiwa na Mwendesha mashtaka wa Serikali (DPP), Biswalo Mganga, Jaji wa Mahakama Kuu Edwin Kakolaki, Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi Jinai wa Mamlaka hiyo, Bertha Mamuya, Mkurugenzi wa Sheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira, Bernad Kongola pamoja na mawakili wa kujitegemea."
#BinagoaUPDATES

No comments