Mwanamuziki Mkenya wa nyimbo za Injili, MCK Official, amewaacha wengi vinywa wazi baada ya kufichua kuwa ni shoga.
Mwimbaji huyo ambaye anasifika sana kwa wimbo wake Mpe Muda, alisema kuwa anajivunia kuhusiana na watu wa jinsia moja na yuko tayari kupigania haki zakeMwanamuziki Mkenya wa nyimbo za Injili, MCK Official, amewaacha wengi vinywa wazi baada ya kufichua kuwa ni shoga.Akizungumza katika mahojiano na Xtian Dela kwenye mtandao wa YouTube, mwanamuziki huyo alidai kuwa aliamua kujitokeza ili kuzipigania haki za wanachama wa LGBTQ .
Kulingana na mwimbaji huyo, ni kinaya kwa Wakristu kudai kuwa wanapendana na wanawatenga wapenzi wa jinsia moja kwa kuwafukuza makanisani, ambayo ni kinyume na mafunzo ya Mwenyezi Mungu.
''Mbona sisi kama wa Wakristu huwa tunawafukuza mashoga. Mbona tuna watenga watu hawa badala ya kuwasaidia," alisema mwanamuziki huyo.MCK alidokezea pia kuwa aliamua kujitokeza ili pia kupigania haki za mashoga kwani muda umewadia kwa watu kufanya mazungumzo.
''Haya ni mazungumzo ambayo yanatakiwa kuangaziwa. Endapo watu hawataki. Endapo itaanza na mimi basi nitaifanya," aliongezea MCK.
MCK alifichua kuwa kuna mashoga wengi ambao huishi maisha ya bandia kwa kuoa wanawake ili kuwa na familia kwa sababu wanaogopa kujitokezaStaa huyo wa Injili anawataka watu kukoma kuwabagua mashoga.
Hata hivyo, bado haijabainika wazi endapo kweli MCK ni shoga ama nikujitafutia tu umaarufu lakini picha zake kwenye mtandao wake wa Instagram zinaibua maswali mengi.
Taarifa ya mwanamuziki huyo inakujia wiki moja tu baada ya mwimbaji mwingine wa nyimbo za Injili kutoka Rwanda, Albert Nabonibo kukiri kuwa ni shogaBibilia takatifu huwa kinyume na mahusiano ya jinsia moja na Wakristu wengi huchukia sana kitendo hicho ambapo baadhi huitambua kama dhambi kubwa.
Katiba ya Kenya pia inapinga mahusiano ya jinsia moja na yeyote anayekiuka sheria hiyo huenda akafungwa jela.

Post a Comment