Kanisa la EAGT lanusurika kubomolewa Arusha
Kanisa la EAGT Sayuni lililopo kata ya Sinoni ,jijini Arusha linalomilikiwa na Askofu Leonard Mwizarubi limenusurika kubomolewa kwa amri ya Mahakama baada ya kubainika kuwa kanisa hilo na wakazi wengine wamevamia na kuweka makazi ya kudumu kinyume cha sheria wakati wakijua eneo hilo linamgogoro na si Mali yao.
Mgogoro huo uliodumu kwa miaka 40 uliwahusisha ndugu wawili ambao ni Nacy Mruo (80) na marehemu Edward Renyasi, waliokuwa wakigombea eneo la urithi ,pamoja na walionunua viwanja na kujenga makazi ya kudumu kwenye eneo hilo .Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi ,Willium Lukuvi, ameyasema hayo jijini Arusha alipokuwa akizungumza na wananchi katika kata hiyo kutekeleza hukumu ya mahakama kuu iliyowataka waliojenga nyumba ndani ya eneo hilo lenye ukubwa wa hekari 8,likiwemo Kanisa la EAGT Sayuni , linaloongozwa na dkt Mwizarubi kubomolewa pamoja na nyumba zao na kuondoka na kuliacha eneo hilo mikononi mwa mmiliki wake ambae ni Nacy Mruo .
Waziri Lukuvi, amesema Mahakama kuu ilimpatia ushindi Nacy Mruo na kuwataka wote waliojenga kuondoka kwa kuwa ni Wavamizi, badala yake serikali imewataka wamlipe Nacy nusu ya bei ya thamani ya ardhi kulingana na ukubwa wa eneo la mtu analomiliki na fedha hizo zitalipwa kupitia Akaunti atakayoifungua mmiliki huyoAmeagiza Idara ya mipango miji ya Jiji la Arusha kushirikiana na kamati ya mgogoro kuhakikisha inawapimia maeneo yao wananchi waliojenga nyumba zao ndani ya eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa hati za umiliki wa ardhi za miaka 99 au kuwapatia Leseni za makazi.
Amesema kuwa atarudi ndani ya mwezi mmoja kuanzia leo ili kuja kutoa taarifa ya malipo wanayotakiwa kulipa waliowekeza ndani ya eneo hilo kulingana na ukubwa wa maeneo yao,ameongeza kuwa katika awamu hii hakuna mgogoro unaoshindikana kutatuliwaAmesema mgogoro huo uliibuliwa Marchi 23,2017 ,siku rais John Magufuli,alipokuja Arusha kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid kutunuku Kamisheni kwa maafisa wa jeshi la ulinzi la wananchi ambapo bibi huyo aliinua bango lenye kulalamikia kutokutekelezwa hukumu iliyompatia ushindi na rais aliagiza swala hilo lipatiwe ufumbuzi .
Waziri Lukuzi,amesema Jana rais akiwa kijijini kwake Chato mkoani Geita, alimtuma akatatue mgogoro huo uliodumu miaka 40 kuanzia mwaka 1979.
Amesema serikali haikuvunja Hukumu hiyo kwa kutowaondoa wavamizi hao badala yake serikali imewataka wananchi hao ambao kisheria ni Wavamizi walipe gharama za ardhi kwa kuwa wameshaishi hapo kwa muda mrefu na wengine hawana uwezo wa kiuchumi lengo la serikali ni kutaka pande zote zinufaike .Aidha ameliagiza kanisa la EAGT nalo kuhakikisha linalipa gharama ya thamani ya ardhi kulingana na ukubwa wa eneo hilo .
Kwa upande wakMwizarubiMwizarubi, amesema kuwa Kanisa lake litalipa gharama hizo zinazodaiwa ,na kuongeza kwamba awali kanisa liliahidi kumjengea nyumba bibi huyo lakini aliliondoa kanisa hilo kwenye mgogoro mwaka 1997!

Post a Comment