Masanja Mkandamizaji atoa ushauri kwa vijana
Mchekeshaji na Mchungaji Emanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji ametoa ushauri na busara zake kwa vijana wa kiume kwamba wakifika miaka 30 na kuendelea, basi wamuombe Mungu na wahakikishe kuna mambo wameyatimiza na hata mengine kuyaacha.
Yasome mambo hayo hapa chini upate kuyajua na kuchukua hatua
Shughuli halali ya kukupa kipato kuweza kuishi haijalishi kiwango gani, sio kuendelea kuwa tegemezi katika umri huo.
Uwe na namba ya simu ambayo sio kila mwezi unabadili badili. Watu wajue wakikuhitaji unapatikana kwa simu fulani.
Uwe na sehemu yako ya kuishi haijalishi kwako, nyumba umepewa urithi au umepanga. Watu wajue unapoishi. Kama hutaki wengi wajue basi angalao watu wako wa karibu.
Kama umefanikiwa kuoa shukuru Mungu na tunza ndoa, kama bado na unatarajia kufanya hivyo basi uwe na mpenzi mmoja anayefahamika na weka mipango ya kuoana wazi hata kama si kesho. Wacha uhuni uhuni.
Acha tabia ya kuchukua mtoto wa mtu na kwenda naye kwako/popote kienyeji na kulala usingizi tena kwa amani kabisa. Kipi kitatokea kama akianguka hapo ulipo naye sasa hivi? Kwao wanakujua? Una mawasiliano yao? Au utakimbia? Acha kufanya mambo kienyeji. Umekua sasa. Eleweka.
Hudhuria shughuli za kijamii. Shiriki mambo ya wanajamii wenzako kama misiba, sherehe, na mengine. Usijifanye wewe uko kivyako vyako, hakuna binadamu anaishi hii dunia kivyake vyake. Mtu ni watu.

Post a Comment