Hii kali:Askofu Ng'ang'a amtishia kumuua mwandishi wa habari

Iwapo unataka maombi ya dharura kutoka kwa muhubiri Askofu James Ng’ang’a, itakubidi sasa utembee guu mosi guu pili hadi kanisani mwake ukamsubiri pale. Hii ni kufuatia simu yake kuchukuliwa na wanapolisi wanaochunguza kisa na ambapo alimtishia kumuua mwanahabari Linus Kaikai.
Soma hapa:

Polisi wanaosaidia katika upelelezi wa kisa hiki wameiambia mahakama kuwa simu hiyo inahusika katika kesi ya mhubiri huyu kumtishia kumtoa uhai Kaikai.

Katika maombi yake James kwa mahakama, mhubiri huyu tata alikuwa ameitaka mahakama kuirejesha simu yake. Mahakama ilikanusha ombi hilo na kusema kuwa simu yake itatumika katika uendeshaji wa shtaka hilo.
Kesi hii imeratibiwa kutajwa Julai 26 na kusikilizwa tarehe 26 mwezi wa Agosti mwaka huu. Ng’ang’a alikana mashtaka ya kutishia mauaji na kuachiliwa huru kwa dhamana ya laki 2 pesa taslimu.

James Ng’ang’a ni mhubiri aliyegongwa vichwa vya habari majuma chache yaliyopita kwa kuwaburuza askofu wake kanisani na kuwatusi mbele ya waumini.

Chanzo:radiojambo.co.ke

No comments