Kanisa la ACK Kenya limekubaliana na ndoa za Jinsia Moja

Kanisa la ACK, limetangaza kuwa alitaidhinisha ndoa za watu wa jinsia moja ila limesema kwamba halitawazuia kushirikia kwenye makanisa yake.

Kauli hii ya ACK, inajiri wiki moja tu baada ya Mahakama Kuu kukataa kuviondoa baadhi ya vipengele katika katiba vinavyoharamisha ndoa za jinsia moja.Kiongozi wa Kanisa hilo Askofu Jackson Ole Sapit akizungumza katika kanisa la all Saints Cathedral , amesema kanisa hilo linazingatia mafundisho ya Bibilia kuhusu ndoa. Amesema kuidhinishwa kwa ndoa za jinsia moja kutaonesha kwamba kanisa hilo linaunga mkono mahusiano hayo.

Askofu Sapit amedokeza kwamba kanisa lazima litumiwa kama kituo cha kurekebisha tabia akitoa wito kwa makanisa mengine kuwaruhusu watu hao kushiriki ibada za Juma Pili

No comments