Bilionea ajuta kumsahau Mungu wakati wa uhai wake

Richard Teo Keng Siang alisema alijutia sana maisha yake ambapo aliishi akikimbizana na kutengeneza mamilioni na kusahau kumfuata Mwenyezi Mungu.Mimi ni mfano mzuri wa jamii ya kisasa. Tangu nikiwa mtoto, nimekuwa na dhana kuwa kuwa na maisha mazuri ni kufaulu maishani. Na kufaulu ni kuwa tajiri. Hivyo ndivyo nilivyoishi," alisema Keng.Daktari huyo alizungumza maneno hayo wakati ambapo alikuwa akiugua saratani ya mapavu na baadaye akafariki mnamo mwaka wa 2012.

Keng alifariki akiwa na miaka 40 huku akiwa tayari akiwa bwenyenye tajika baada ya kuunda mamilioni ya pesa kwenye taaluma yake.

Utajiri huo ulimfanya kuwa mpenzi mkuu wa maisha ya kianasa ambapo wakati mwingi alikuwa akishiriki uendeshaji magari kwa kasi."Kinaya cha maisha ni kuwa licha ni mali yote niliyokuwa nayo; magari, nyumba na zingine zote nilifikiri zingenipa furaha, lakini sivyo," alisema.

No comments