"watumishi wa serikali kuendekeza vitendo vya rushwa"Askofu wa Anglikana alisema

Dodoma:
ASKOFU wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Kati, Dk.Dikson Chilongani amesema kuwa licha ya kuwa serikali inapambana na rushwa lakini hali hiyo bado ipo na kwa kiwango cha juu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Alitoa kauli hiyo jana katika ibada ya sikukuu ya Kuzaliwa Yesu Kristo iliyofanyika kanisa kuu Jijini Dodoma.

Akihubiri kanisani hapo alisema kuwa ni aibu kwa watumishi wa serikali kuendekeza vitendo vya rushwa licha ya serikali kupiga vita vitendo vya rushwa na ufisadi.
Dk. Chilongani alisema kuwa kwa sasa rushwa zinaendelea kufanyika katika ofisi za Umma huku jina linalotumika kudai rushwa ni “support Docoment” jambo ambalo linakwemisha utendaji wa kazi kwa ufanisi.

“Hivi karibuni nilisafiri kwenda nje ya nacho cha kusikitisha nilipofika uwanja wa ndege wa Dar es saalam, nilipokelewa na wahudumu ambao ni watumishi wa serikali licha ya kuwa sikuwaomba msaada wowote, wa kunisindikiza au kufunga zipu ya begi langu lakini waliniomba hela ya soda ambayo ni rushwa,” alisema Askofu Dk. Chilongani.

Katika mahubiri yake askofu alisema kuwa vita ya rushwa isiwe ya mtu mmoja au serikali pekee bali iwe ya watanzania wote na kama rushwa haitapigwa vita na watu wote ni dhaili kuwawatu wanyonge hawatapata haki zao.

Katika hatua nyingine askofu amekemea baadhi ya askari polisi ambao wanaendekeza vitendo vya rushwa kwani kuendekeza vitendo hivyo ni kupotosha ukweli.

“Rushwa haikuanza leo imekuwepo kwa muda mrefu hata kipindi cha Yesu Yuda aliongwa vipande 30 ili ams

No comments