Kumbe Sheikh ndiye aliyejenga hospitali ya MUHIMBILI :Historia fupi

Anaitwa Sewa Haji Paroo Alifika Zanzibar Akitokea Katika Miji Ya Bhuj Na KutchNa Mnamo Mwaka 1852 Alifungua Duka La Bidhaa Mbalimbali Huko Zanzibar, Mnamo1860 Akafungua Duka Lingine Kubwa Bagamoyo Na Kuweka Makazi Yake, Biashara Zake Zikawa Kubwa Na Kuwa Tajiri Mkubwa Sana, Alisaidia Watu Wote Bila Kujali Rangi, Dini Wala Kabila Zao, Alinunua Majengo Mengi Na Kuyafanya Maeneo Ya Watu Wasiojiweza, Alijengaja Mashule Na Hospitali Kadhaa, Katika Mji Wa Mzizima {Leo Inaitwa Dar es Salaam}.

Alijenga Hospitali Akaiita Sewahaji Hospitali Ikitoa Huduma Bure, Mnamo February 1897 Sheikhe Sewa Haji Paroo Alifariki Dunia, Ilikuwa Ni Huzuni Na Simanzi Kwa Wakazi Wa Bagamoyo Na Mzizima Kwa Kuondokewa Na Sheikhe Sewa Haji Aliependwa Sana, Baada Ya Kufa Kwake Wakoloni Baadaye Wakabadilisha Jina Kutoka Sewahaji Hospital Na Kuiita Princess Magreth Hospital, Na Mnamo 1963 Iliitwa Muhimbili Hospital, Na Mojawapo Za Wodi Inaitwa SEWA HAJI,
Kazi ya Waislamu ni kubwa katika jamii.

No comments