Ajabu,Mabikira 'watakatifu' wanaoolewa na Yesu katika Katoliki leo!
Lakini hata ndani ya Ukatoliki, ada hii inayofahamika kwa kingereza kama consecrated virgins si maarufu- na waumini wachache wanafahamu juu ya mabikra hao- moja ya sababu ni kuwa ada hiyo iliruhusiwa kwa uwazi na kanisa chini ya miaka 50 iliyopita.
Katika sherehe ya wakfu ama harusi, mwanamke bikra ambaye huvaa shela jeupe- hula kiapo cha maisha cha kutojihusisha na mahusiano ya kimapenzi
na kutokufanya ngono.
Wanawake hao pia huvaa pete za ndoa - ambayo huwa ni alama ya kufunga uchumba ama ndoa na Kristo.
"Mara nyingi naulizwa: 'Kwa hiyo, umeolewa?'" anasema bi Hayes. "Kawaida huwajibu kuwa mimi ni sawa tu na wanawake watawa (masista) wa kanisa, na nimejitoa kwa Kristo kwa moyo wote, tofauti mie naishi nje na watu wa kawaida."
Tofauti na masista, mabikra watakatifu ama wake wa Yesu, hawaishi kwenye makao maalumu ya kanisa ama kuvaa nguo maaalumu; wanaishi maisha ya kawaida, wanafanya kazi na wanijetegemea kwenye kuendesha maisha yao ya kila siku.
Post a Comment