Hatimaye George Pell: Kadinali wa kanisa katoliki hatiani

Pell mwenye umri wa miaka 77 anatarijiwa kuhukumiwa siku ya Jumatano, lakini mawakili wake wanasema kua watakata rufaa hatia hiyo.
Kiongozi huyu wa kanisa aliyekua anashikilia nafasi ya Muweka hazina, na ni miongoni mwa viongozi wenye nguvu Zaidi kanisani,
Kesi yake ilisikilizwa mara mbili mwaka jana,
Amekutwa na hatia, ikiwemo ya kumuingilia mtoto chini ya miaka 16, na hatia zingine nne za kuwafanyia vitendo visivyo vya kawaida watoto wa chini ya miaka 16.
Kanisa katoliki duniani kote kwa miaka ya hivi karibuni, limekubwa na kashfa ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto, na kudaiwa kuwa wamekua wakificha masuala hayo.
Kwa wakati wote kadinali Pell amekanusha kuhusika na matukio yote , kwa sasa yupo katika mapumziko marefu wakati wote wa kesi hii ikiendelea.
Mahakama ilisikiliza nini ?
pellHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionkesi ya Pell imevutia watu wengi Duniani
Pell alikua katika mwaka wake wa kwanza katika kanisa huko Melbourne mwaka 1996 alipowafanyia unyanyasaji watoto , baada ya kuwaambia kuwa walikunywa mvinyo wa kanisa, aliwalazimisha kumfanyia vitendo visivyofaa kama adhabu yao.
Kanisa lilipata fursa ya kusikia ushahidi kutoka kwa mmoja wa wahanga wa unyayasaji huo, muathiriwa mwingine tayari amekufa.
Hatia za Pell sasa zimevutia umakini wa wetu wengi ikizingatiwa , Papa Francis ameanza jitihada za kupambana na tatizo hili ikiwemo mkutano uliofanyika wiki iliyopita .

4 comments: