Barua ya Albert Einstein kumhusu Mungu ,je aliamini kuwa Mungu yupo???

Albert Einstein, ambapo anajadili suala la dini na imani, imeuzwa kwenye mnada kwa bei ya karibu $2.9m (£2.3m).
Bei hiyo imepita makadirio.
Barua hiyo ambayo kwa utani imekuwa ikiitwa "Barua ya Mungu" aliiandika Einstein mwaka 1954 na ilitarajiwa kuuzwa $1.5m (£1.2m) mnadani New York.

Einstein aliamini kwamba Mungu yupo?

Einstein alikuwa kwenye kundi la watu ambao imani yao huitwa Pantheism kwa Kiingereza.
Ni watu wanaoamini kwamba "Mungu ni kila kitu".
Mara kadha, alionyesha mtazamo huu kwenye mawasiliano yake na Rabbi Herbert S. Goldstein, "Ninaamini katika Mungu wa Spinoza, ambaye anajidhihirisha kupitia upatanifu wa vitu vyote vilivyomo, si katika Mungu anayejishughulisha katika hatima na matendo ya binadamu."
Pantheism kwa njia rahisi zaidi ni imani kwamba kila kitu humwakilisha Mungu. Wenye kufuata imani hii mara nyingi hueleza kwamba Mungu ni vitu vyote vilivyopo, au kwamba mambo na vitu vyote ni Mungu. Kwamba kila ukionacho ni sehemu ya Mungu.

2 comments: