Askofu mkuu wa iran: amlaani Rais Trump kwa kuhamishia ubalozi jerusalem
Askofu Mkuu wa Iran: Marekani haina uwezo wa kukabiliana na mshikamano wa taifa la Iran
Askofu Mkuu wa Wakristo wa Kiarmenia wa Tehran na kaskazini mwa Iran amesema kuwa, karibu miaka 40 sasa taifa la Iran limesimama imara kukabiliana na vikwazo kwa nguvu zake zote hivyo, Marekani na mabeberu wengine wa dunia hawana uwezo wa kukabiliana na umoja na mshikamano wa taifa la Iran.
Askofu Sebuh Sarkisian amesisitiza kwamba, hakuna vikwazo vyovyote vinavyoweza kulipigisha magoti taifa imara la Iran na kufafanua kuwa, nchi za kibeberu zinakanyaga haki za kimsingi kabisa za watu duniani na ni vitendo hivyo vya waistikbari ndivyo vinavyoandaa mazingira ya kuamka mataifa ya dunia.
Askofu huyo Mkuu wa Wakristo wa Kiarmenia wa Iran amelaani hatua ya kiadui ya rais wa Marekani ya kuuhamishia jerusalem ubalozi wa nchi hiyo uliokuweko Tel Aviv huko Palestina na kusema: Hatua hiyo ya serikali ya Marekani imeleta wimbi jipya la umwagaji damu na wakimbizi, hivyo viongozi wa nchi nyingine duniani wana wajibu wa kuongeza juhudi za kuleta uadilifu na amani ulimwenguni.
Vile vile amesema, wafuasi wa dini za Mwenyezi Mungu, iwe ni Waislamu wa Kisuni na Kishia au Wakristo wa Orthodox na Protestant na wafuasi wa dini nyingine, wanaishi pamoja kwa usalama na amani chini ya kivuli cha Jamhuri ya Kiislamu na wanapata haki zao zote za kiraia kwa usawa bila ya unyanyasaji wala ukandamizaji wa aina yoyote ile.

Post a Comment