Bernadino KasambulaAamua kuishi juu ya Kanisa akidai ardhi ni yake alidhulumiwa
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamume mmoja mkoani Geita aliyejulikana kwa jina la Bernadino Kasambula, ameamua kuishi juu ya paa la kanisa kwa siku bila kushuka kwa kile alichokieleza kuwa ni kudhulumiwa ardhi na familia aliyodai kuachiwa urithi na marehemu babu yao.
Tukio hilo limevuta hisia za watu wengi kufuatia msimamo wake wa kutoshuka juu ya paa mpaka haki ipatikane kwa maelezo kuwa walipokonywa ardhi hiyo baada ya kufungwa miaka 30 jela.
Licha ya Jeshi la Polisi kufika eneo la tukio na kumtaka kushuka, Bernadino Kasambula aliendelea na msimamo wake wa kubaki juu ya Kanisa.
Bernadino amesema eneo hilo na maeneo mengine zaidi yenye ekari 15 yana mgogoro na familia ya Bi Helen Bajimo na kwamba uamuzi wake wa kukaa juu ya paa ni kuzuia Kanisa lisiendelee na ujenzi.
Post a Comment