Diamond Platinumz akili kuwa nyimbo anazo ziimba Mungu hapendezwi nazo




Msanii wa bongo Diamond Platinumz amepunguza kasi yake kwenye kazi zake za kimuziki tangu alipokamatwa kwa kupachika mitandaoni picha zilizodaiwa kukiuka maadili.

Baba huyo wa watoto watatu ameonekana kuwa na mtazamo mpya baada yake kuonekana kujutia baadhi ya njia alizozichagua maishani.
Akizungumza alipokuwa akizindua kipindi chake kipya cha ‘Nyumba ya Imani’, Diamond alisema hatakuwa mwimbaji maisha yake yote.

Kulingana naye, anafanya muziki ili apate pesa za kufanya biashara kubwa.

Platinumz alikiri kuwa anajua Mungu hapendi miziki ya kidunia na kuwaomba wasanii wenzake kujaribu kuwa watu wema.

“Ndugu zangu Waislamu, mtambue kuwa Mungu hapendi kile tunachokifanya. Tujitahidi kufanya mambo mazuri na kuyaepuka yale mabaya.” Diamond alisema.
Mkuu huyo wa kituo cha runinga cha Wasafi TV alisema kuwa ndoto yake ni kuwa mfanyibiashara, akipanga kuachana na muziki baada ya kupata pesa za kutosha.

“Ndoto yangu ni kuwa mfanyibiashara na sio kuangazia muziki maisha yangu yote.” Platinumz alieleza.

Msanii huyo aliongeza kuwa alikuwa binadamu na mwenye uwezo wa kuteleza na kufanya makosa.

Diamond alisema kuwa taaluma yake imemtia kwenye majaribu mengi na nyakati zingine huwa anakuwa mdhaifu na kukiuka imani ya dini yake.


No comments