Daddy Owen na mkewe kuandaa sherehe kubwa ya kumtarajia mwanao wa pili

Mwimbaji wa humu nchini, Owen Mwatia almaarufu Daddy Owen pamoja na mkewe, Farida Wambui Kamau wanamtarajia mwana wao wa pili.

Fununu zilizofikia TUKO.co.ke mnamo Jumanne, Mei 22 ni kuwa wanandoa hao wana mpango wa kuandaa sherehe za kumtaraji mwana wao wa pili maarufu kama 'Baby Shower', sherehe inayotarajiwa kuwa ya kukata na shoka.

Daddy Owen na mkewe kuandaa sherehe kubwa ya kumtarajia mwanao wa pili
Daddy Owen na mkewe kuandaa sherehe kubwa ya kumtarajia mwanao wa pili PICHA: Hisani
Habari kutoka kwa wandani wake mfalme huyo wa Kapungala zilifichua kuwa Farida alikuwa ameshataka huduma za mpishi maarufu jijini kushughulikia keki na vinginevyo.

Daddy Owen husemekana kukutana na Kamau mnamo mwaka wa 2012 kabla ya kumposa mwaka wa 2014.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Daddy Owen na mkewe kuandaa sherehe kubwa ya kumtarajia mwanao wa pili
Daddy Owen na mkewe kuandaa sherehe kubwa ya kumtarajia mwanao wa pili PICHA: Hisani
Wamebarikiwa na mtoto mmoja, na wanamtarajia wa pili.

Kabla ya harusi yao ya 2016, wawili hao walikuwa tayari na mwana wao wa kwanza.

No comments