Mwanamuziki wa nyimbo za injili Size 8 apata kazi nyingine!

Linet Munyali almaarufu Size 8, amekuwa akiona mkono wa Mungu tangu alipoacha kuimba nyimbo za dunia.

Siku kadhaa baada ya kupata kazi ya runinga kuendesha kipindi cha injili, mama huyo wa mtoto mmoja amepata kazi nyingine ya utangazaji katika radio moja ya humu nchini.
Kwa furaha kuu Size 8 katika mtandao wa kijamii Jumanne, Mei 15 alitangaza habari hiyo njema.

Atakuwa anaendesha shoo Kubamba Radio inayofahamika kama Kvibes916 na ambayo itakuwa anaanzia saa nne asubuhi hadi saa saba mchana

Shoo hiyo itaanzia Ijumaa Mei 18 na itakuwa inaendelea kila ijumaa kila wiki.

“Ninafuraha kuwafahamisha kuwa kuanzia Ijumaa, Mei 18 na kila Ijumaa kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa saba mchana shoo itakuwa ni KVIBES916 Kubamba Radio,” aliandika.

Kulingana na Size 8, alipata kazi hiyo bila kutarajia kwa sababu hajawahi kufikiria kuwa mtangazaji katika radio.

Alimshukuru Mungu kwa kupanga maisha yake na kumpa makuu asiyotarajia. Amejiunga na msururu wa wanamuziki wa nyimbo za injili waliojiunga na radio akiwemo Kambua na Danco.

No comments