MADRID ILIKOSA UJASIRI DHIDI YA MAN CITY MSIMU ULIOPITA
Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti alisema Jumatatu timu yake ilicheza bila ujasiri au utu wakati Manchester City ilipowaondoa kwenye Ligi ya Mabingwa msimu uliopita, kabla ya pambano lingine na mabingwa hao wa Uingereza.
Kikosi cha Pep Guardiola kiliizaba Madrid kwa jumla ya mabao 5-1 katika nusu fainali ya msimu uliopita na Ancelotti aliwataka wachezaji wake kuonyesha nguvu zaidi kiakili wakati huu.
Washindi mara 14 wa Madrid wanawakaribisha mabingwa watetezi City katika uwanja wa Santiago Bernabeu siku ya Jumanne katika mchuano mkali wa robo fainali ya mkondo wa kwanza.
Tulicheza bila ujasiri, bila utu — ujasiri na utu ni msingi katika aina hii ya mchezo, tulikosa katika mechi ya mkondo wa pili,” Ancelotti aliambia mkutano wa wanahabari.
Baada ya sare ya 1-1 katika mji mkuu wa Uhispania Madrid walichapwa mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Etihad.
Post a Comment