BEKI KUSHAMBULIWA NA WATU WASIO JULIKANA


 Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imethibitisha kifo cha beki wake Luke Fleurs (24) kilichotokea jana usiku Johannesburg Afrika Kusini kwa kushambuliwa kwa kupigwa risasi.

Tukio hilo limetokea akiwa katika kituo cha kuwekea mafuta jijini Johannesburg ambapo kwa mujibu wa msemaji wa Polisi wa Gauteng, Mavela Masondo anasema shuhuda anadai wauaji walimuamrisha Luke ashuke kwenye gari kabla ya kumpiga risasi na kumuua.

Luke Fleurs aliyekuwa na ndoto ya kutwaa taji la Ligi Kuu Afrika Kusini akiwa na Kaizer, alijiunga na timu hiyo Oktoba 2023 akitokea Super Sport aliyodumu nayo kwa miaka mitano.

Luke alizaliwa Machi 3 2000 na alianza kucheza soka 2013 alipojiunga na academy ya Ubuntu Cape Town iliyomfungulia njia ya soka lakini bahati mbaya anaponywa uhai akiwa hajaichezea Kaizer Chiefs mechi yoyote ya ushindani.

No comments