Samatta aomba asichezee Taifa Stars
KAIMU Kocha Mkuu wa Stars Hemed Morocco ametangaza kikosi cha wachezaji 23, mshambuliaji Mbwana Samatta na beki Dickson Job wametemwa.
Huku Mshambuliaji wa Yanga Sc Clement Mzize na beki wa Simba Kennedy Juma wakijumuishwa ndani ya kikosi cha wachezaji hao ambao wataingia kambini Machi 17 mwaka huu
Kikosi hicho ni makipa, Aishi Manula (Simba), Aboutwaleeb Mshery (Yanga) na Kwesi Kawawa (Syrianska FC, Sweden) mabeki ni Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca (Yanga).
Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Haji Mnoga (Aldershot Town, Uingereza, Mohammed Hussein na Kennedy Juma (Simba) Novatus Miroshi (Shakhtar Donestsk, Ukraine na Miano Danilo (Villena CF, Hispani)
Viungo ni Feisal Salum na Yahya Zaydi kutoka Azam FC, Mudathir Yahya kutoka Yanga Sc, Morice Michael kutoka RFK Novi Sad ya Serbia, Himid Mao kutoka Telaea El Gaish SC ya Misri na Tarryn Allarakhia kutoka Wealdstone ya Uingereza
Washambuliaji ni Mzize, Simon Msuva (Alnajmah FC, Saudi Arabia), Kibu Denis (Simba), Abdul Suleiman (Azam FC), Ben Starkie (Ilstone Town, Uingereza) na Charles M’mombwa ( Australia).
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars Hemedi Morocco, amesema Wachezaji walioitwa katika kikosi hicho ni mchanganyiko wa vijana na wachezaji wenye uzoefu mkubwa
Morocco amesema Stars inaingia kambini Machi 17 na 18 mwaka huu huku kikitarajia kuondoka kuelekea nchini Azerbaijan ambako watacheza mechi mbili za FIFA Series 2024
“Tutakuwa na mechi mbili za kirafiki tutacheza Machi 22 na 25, mwaka huu dhidi ya Bulgaria na Mongolia, baada ya hapo wachezaji watarejea haraka kwa ajili ya majukumu mengine.
Tumechanganya baadhi ya wachezaji kuwapa nafasi vijana na sura mpya kwa lengo la kutengeneza timu imara ijayo,”—
Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars Hemedi Morocco
Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limeweka wazi kuwa mshambulijai Mbwana Samatta anayekipiga katika timu ya PAOK nchini Ugiriki aliomba asijumuishwe kwenye kikosi cha Taifa Stars kitakachocheza mechi za FIFA Series 2024 dhidi ya Bulgaria na Mongolia, Machi 22 na 25 mwaka huu nchini Azerbaijan.
Post a Comment