MFANYABIASHARA AUNGANA NA MAMA SAMIA KUNUNUA MAGOLI SIMBA NA YANGA


 Mfanyabiashara wa Madini Hussein Makubi maarufu kama Mwananzala ameungana na Rais Samia Suluhu Hassan kuongeza  hamasa kwa Simba na Yanga katika michuano ya Kimataifa.

Makubi ametangaza kuwa kwa sababu Rais Samia atatoa Tsh milioni 10 kwa kila goli kwa Simba na Yanga katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika yeye atatoa Tsh milioni 10 kwa kila kwa Simba na Yanga endapo watashinda.

Simba atacheza mchezo wake wa kwanza wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika siku ya Ijumaa ya March 29 katika uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Al Ahly ya Misri wakati Yanga watacheza dhidi ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini Jumamosi ya March 30 2024.

No comments