Kwa mipango hii, Yanga lazima wafike nusu Fainali
... 🗣️ 𝙔𝘼𝙉𝙂𝘼 𝙉𝙐𝙎𝙐 𝙁𝘼𝙄𝙉𝘼𝙇𝙄 (𝘾𝘼𝙁)
Kiungo wa Al-Ahly aitabiria makubwa Yanga SC kwenye michuano ya CAF-CL.
"(Al-Ahly) Tulikuwa tunaangalia mechi yao iliyopita (Yanga SC 4 - 0 Belouizdad), kila mmoja alishangaa kwa kiwango ambacho Yanga walikionesha kwenye Mchezo huo"
"Ukikumbuka kiwango chao tulipokutana nao (Yanga 1 - 1 Al-Ahly) + hiki walichofanya kwa CR Belouizdad 🇩🇿 utaona hii timu ina uwezo mkubwa kwa sasa Africa sitashangaa kuona wanacheza nusu fainali au hata fainali (CAF-CL) kama wakikutana na timu ya Kawaida kwenye hatua ya robo fainali"
"Kitu ambacho kimewapa nguvu ni kuwa na wachezaji bora sana ambao wamekuwa wakiamua matukio magumu uwanjani mfano Djigui Diarra. Diarra ni mchezaji muhimu sana kwenye timu yetu ya taifa ya Mali 🇲🇱 vivyohivyo kwa Yanga"
"Nimekuwa nikiifatilia Yanga muda mrefu kupitia kwa Djigui Diarra ni timu nzuri inayocheza mpira mzuri wakuvutia"
©️ Aliou Dieng
Kiungo wa Al-Ahly Via Mwanaspoti
Post a Comment