GRAHAM POTTER KUHUSISHWA NA MANCHESTER UNITED


 Bilionea wa Uingereza Sir Jim Ratcliffe amekutana na kocha wa zamani wa Chelsea, Graham Potter, kuchukua nafasi ya Erik ten Hag katika klabu ya Manchester United.

Ratcliffe anatazamiwa kuchukua udhibiti wa uendeshaji wa soka huko United akiwa na asilimia 25 ya hisa zenye thamani ya pauni bilioni 1.3.

Kulingana na The Sun, anazingatia Potter kama mbadala wa Ten Hag huko Old Trafford.

Ingawa hatamtimua Ten Hag mara moja, Ratcliffe atalazimika kutathmini hali ikiwa hali duni ya Mashetani Wekundu itashindwa kuimarika.

United iliondoka Ulaya kabisa wiki hii baada ya kumaliza mkiani mwa kundi lao la Ligi ya Mabingwa.

No comments