Advertisement

Responsive Advertisement

YANGA MAMBO SAFI SASA ⚽️ 🔥


 Tanga ni yellow and green! Yanga kwao ilikuwa muhimu zaidi alama 3 na approach nzuri imewapa matokeo, waliingia kwa 4 - 2 - 2 - 1 dhidi ya Coastal Union ambao waliingia kwa plan ya 4 - 5 - 1 kujilinda zaidi.


Kazi nzuri sana kwa Aucho kwa kiufundi zaidi alikuwa anazuia njia za mpira 🔥 Gwalala alikuwa na game nzuri sana na alimpa maswali mengi Mudathir🙌 akishirikiana na Lucas Kikoti pale kwenye midfield.


Coastal Union walikuwa na wakati mzuri sana kipindi cha kwanza, approach ya kucheza chini sana na kuzigawanya vizuri 90, lakini Mwalimu Miguel Gamondi alifanya mabadiliko ya Mauya na Moloko! Impact yake ilikuwa nzuri sana.


KI Aziz, Nzengeli na Zouzoua walikuwa wanaleta balance nzuri kwenye midfield, Ajib alikuwa anatoa darasa huru leo 🔥 lakini quality ya Yanga kwa ingizo la Mzize ilikuwa sahihi sana! Tough game sana.


Coastal Union wanawaza sana kuzikosa alama 3 ambapo alama 1 ilikuwa muhimu kwao, Yanga walikuwa bora sana kuliko Coastal Union! Mpira unakupa kwa kadri ulivyojipanga, muhimu zaidi kwa Yanga ni kuwa siku hizi inaendelea kuvuna alama ugenini.


Muhimu ni kuwa kimahesabu kwa Yanga imepata alama 3 na inaongoza Premier League! Its football its easy!


FT: Coastal Union 0-1 Young Africans

Post a Comment

0 Comments