Walinzi wa kampuni ya Samike Security Company iliyopo Geita wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua Shabiki mkubwa wa Yanga aitwae Alex Mayaya mwenye umri wa miaka 40 baada ya kuhisiwa kuwa ni mwiz.
Tukio hilo lilitokea Tarehe 5,Novemba 2023 majira ya usiku mara tu baada ya mtanange wa Simba na Yanga.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la ukatili dhidi ya Alex ambaye alikuwa mfanyabiashara.
Mara tu baada ya mechi kuisha na Yanga kupata ushindi Alex alishangilia kupita kiasi huku akiwa amelewa sana kisha akaenda kwenye duka lake akatoa matairi mawili ya pikipiki na kwa babati mbaya duka lake linaendeshwa na kijana,hivyo walinzi wa pale walikuwa hawamfahamu vizuri bwana Alex,mara baada tu ya kuhisi ni mwizi wakamkamata na kumshambulia sana na rungu hivyo kupelekea umauti wake.
Stream mechi live na app ya Binago tv
.png)
0 Comments