Advertisement

Responsive Advertisement

𝗠𝗡𝗔𝗠𝗨𝗢𝗡𝗘𝗔🦁


 Wanasimba wengi wamechachamaa wanamlaumu Murtaza Mangungu na kumtaka AJIUZULU, vilevile kwa Try Again.


Kwa Mangungu ndugu zangu mnamuonea tu bure. Kwa mujibu wa katiba ya Simba soorts club, Mangungu hana SAUTI kwenye Bodi ya Simba yeye ni mjumbe tu japo ana jina lenye TITLE kubwa 'Mwenyekiti' lakini kiuhalisia hana mamlaka hayo ya uenyekiti.


Ukitaka uamini hilo tazama kwenye matukio mengi makubwa, huwezi kumuona, wenye SAUTI ni Try Again, Mo Dewji na CEO Kajula ambaye ameajiriwa na bodi.


𝗠𝗳𝗮𝗻𝗼 :


Kwenye Simba day aliyetakiwa kusoma ripoti ya klabu kwa Rais, Samia Suluhu alitakiwa kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu lakini aliyewasilisha ni Mo Dewji ambaye cheo chake cha Urais wa heshima hakipo kwenye katiba.


Uenyekiti wa Mangungu Simba SC ni wa kufungua vikao na kufunga, hana sauti mbele ya muwekezaji na bodi yake.


Mbuzi wa kafara 🐐

.

.

𝗠𝗮𝗮𝗻𝗱𝗮𝗺𝗮𝗻𝗼 :


Wazee wa klabu ya Simba na wanachama wengine wa Simba wakiongea na wanahabari wamesema watafanya MAANDAMANO hadi Viongozi wa Simba SC, Murtaza Mangungu na Try Again WAJIUZULU.


Wametoa saa (24) wajiuzulu kwa hiyari yao.


NB : Simba anapaswa ashinde leo kwa ushawishi, bila hivyo yajayo yanasikitisha.


Ukizingatia ligi inasimama kwa wiki mbili kupisha FIFA International break.

Post a Comment

0 Comments