WAZAZI WA LUIS DIAZ WATEKWA COLOMBIA


 Ripoti kutokea Colombia zinaeleza kuwa wazazi wa mshambuliaji wa Liverpool Luis Diaz walitekwa nchini humo lakini hadi sasa Mama amepatikana.


Wakati wakielekea nyumbani kwao wawili hao walizingirwa na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki. Tukio hilo limetokea kwenye kituo cha mafuta.


Kupitia mtandao wa X, Rais wa Colombia Gustavo Petro amethibitisha kuwa Polisi wamefanikiwa kumuokoa mama Bi.Cilenis Marulanda lakini baba hajulikani alipo.


Naye Mkurugenzi wa Polisi nchini Colombia Jenerali William Salamanca ameapa kutumia kila njia na namna ili kumpata Baba wa Diaz.


Shirikisho la soka la Colombia limeeleza kusikitishwa kwake na kitendo hiko na kuhimiza mamlaka kumuokoa baba huyo.


Nayo klabu ya Liverpool imesema kuwa inatumaini suala hili litamalizika kwa usalama, na kwa sasa jukumu lao ni kutuliza hali ya mchezaji wao. 


No comments