HIFADHI YA SERENGETI YAPATA TUZO
Hifadhi ya Taifa Serengeti imeshinda tuzo ya hifadhi bora na mwaka barani Afrika kwa mwaka 2023(Africa's leading National Park 2023) ,hifadhi hii ya Serengeti imeweza kuchukua tuzo hii kwa mara ya tano mfululizo
15,oktoba,2023 tuzo hiyo ilitolewa na World Travel Awards katika falme za kiarabu na kupokelewa na mkuu wa kanda ya magharibi kamishna Msaidizi mwandamizi wa uhifadhi Izumbe Msindai kwa niaba ya Shirika la Hifadhi Tanzania(TANAPA)
Hifathi ya Serengeti inakuwa hifadhi bora mwaka 2019,2020,2021,2022 na 2023
Hivyo kupelekea hifadhi ya Serengeti kuwa bora sana barani Afrika kutokana na uwekezaji mkubwa wa serikali kwenye sekta ya Utalii
Post a Comment