Aliyekataa goli la Singida Fountain gate afungiwa michezo (5) na Bodi ya ligi.
Hizi hapa Adhabu zilizotolewa na TFF
𝗣𝗿𝗶𝘀𝗼𝗻𝘀 𝗱𝗵𝗶𝗱𝗶 𝘆𝗮 𝗦𝗶𝗺𝗯𝗮 :
Mwamuzi msaidizi namba mbili wa mchezo uliowakutanisha Prisons FC dhidi ya Simba SC, Nestory Livangala (Iringa) ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitano (5) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu katika mchezo uliotajwa hapo juu.
Katika mchezo huo Simba SC iliibuka na Ushindi wa magoli (1-3) dhidi ya Tanzania Prisons katika Dimba la Sokoine Mbeya
𝗦𝗶𝗻𝗴𝗶𝗱𝗮 𝗱𝗵𝗶𝗱𝗶 𝘆𝗮 𝗦𝗶𝗺𝗯𝗮 :
Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemwondoa Mwamuzi Msaidizi namba mbili wa mchezo wa Singida Fountain Gate dhidi ya Simba SC, Abdallah Bakenga kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitano, kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu katika mchezo tajwa.
𝗜𝗵𝗲𝗳𝘂 𝗱𝗵𝗶𝗱𝗶 𝘆𝗮 𝗬𝗮𝗻𝗴𝗮
Klabu ya Yanga imetozwa faini ya shilingi milioni mbili kwa makosa (2)
◉ Tsh Million 1 kwa kosa la naashabiki wake kurusha chupa za maji uwanjani
◉ Tsh Million 1 kwa kosa la maofisa wa klabu ya Yanga wa benchi la ufundi kuonekana wakipinga maamuzi na kumzonga mwamuzi wa akiba.
◉ Kocha wa Ihefu, Zuberi Katwila amepigwa faini ya Tsh million 1 kwa kosa la kuwaambia watu wa huduma ya kwanza kutembea polepole wanapowatoa kwenye pitch wachezaji wa Ihefu ili kupoteza muda.
Pia, afisa habari wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe amepigwa faini ya Tsh Million 1 kwa kosa la kumkejeli mwamuzi, Tatu Malogo kwenye mtandao wa kijamii baada ya mechi ya Singida dhidi ya Simba SC.
Alikamwe alipost picha ya Tatu Malogo kisha akaweka wimbo wa 'MAOKOTO'
𝗗𝗼𝗱𝗼𝗺𝗮 𝗷𝗶𝗷𝗶 𝗱𝗵𝗶𝗱𝗶 𝘆𝗮 𝗔𝘇𝗮𝗺
Klabu ya Azam FC imepewa onyo baada ya kuchelewa kuwasili uwanjani kwa dakika (8).
Post a Comment