Simba SC wasipokuwa makini huenda wakaukosa ubingwa wa ligi kuu hata kwa misimu miwili ijayo.

Klabu ya Simba SC wasipokuwa makini huenda wakaukosa ubingwa wa ligi kuu hata kwa misimu miwili ijayo !

 Uongozi wa klabu ya Simba SC ulithibitisha umeanza project mpya ya kuingiza damu changa kikosini,, Wakasajili Wachezaji wafuatao msimu huu ;

01 - 🇲🇼 Peter Banda 
02 - 🇹🇿 Jimmyson Mwanuke
03 - 🇸🇳 Pape Ousmane Sakho
04 - 🇹🇿 Yusuph Mhilu
05 - 🇲🇱 Sadio Kanoute
06 - 🇹🇿 Kibu Denis
07 - 🇨🇩 Henock Inonga
08 - 🇹🇿 Abdulswamadu
09 - 🇲🇼 Duncan Nyoni
10 - 🇿🇲 Clatous Chama

Kosa limeanzia hapo, inaonekana project haikuwa imewekewa misingi mizuri,, Baada ya msimu mmoja tu tayari uvumilivu umeanza kuwashinda, inatajwa kwenye dirisha kubwa wataachwa si chini ya Wachezaji (10+) katika kikosi cha Simba.

Wakati Simba wakiendelea kujitafuta, wenzao Yanga SC wanahitaji maboresho machache tu ili kuwa na kikosi imara zaidi.

Project ya vijana inahitaji muda na uvumilivu, aliyeanzisha project hii ya Simba itakuwa alikuwa hajui au presha inawasukuma viongozi kujikuta wanalazimika kuivunja.

Unaweza kuacha Wachezaji (10+) ukafanikiwa katika scouting yako kupata mbadala ya Wachezaji uliowaacha, pia inaweza kuwa kinyume chake ukazidi kupotea kabisa.

Believe me ; Kama Yanga ingeendelea kuwa ileile ya msimu uliopita muda huu Simba hii hii inayoonekana mbovu ingekuwa imechukua ubingwa.

Tofauti ya msimu huu ni moja tu, Yanga wameimarika kuliko vilabu vingine na kupelekea kuona kama Simba ina matokeo mabovu sana kitu ambacho si kweli.

Msimu uliopita Simba walitwaa ubingwa wakiwa wamepoteza michezo (2), mpaka sasa msimu huu wamepoteza michezo (2) tu kama msimu uliopita.... 

Yanga kuimarika ndio kumeleta utofauti, Viongozi wa Simba hawataki kukubali kuwa gari likipanda mlima lazima lishuke.

Katika miaka (4) ya kukosa ubingwa, Yanga walishawahi kusajili wafungaji bora wa Rwanda na Uganda,, Juma Balinya na Sarpong lakini ligi yetu ikawashinda.

Kusajili ni jambo moja na ku-perform ni jambo jingine,, Unaweza ukaacha Wachezaji 20, ukasajili 20 lakini ukazidi kuanguka zaidi.

🔍 Tom cruz
TANGAZA NASI KWA GHARAMA NAFUU TUPIGIE, 0679663340

No comments