MWANAMKE AUAWA NA MUMEWE KISA ALICHELEWA KURUDI NYUMBANI
MWANAMKE MAARUFU MWANZA AUAWA NA MUMEWE KWA KUMPIGA RISASI SABA KICHWANI, ALICHELEWA KURUDI NYUMBANI
Kutoka jijini Mwanza Mwanamke maarufu jijini humo anaefahamika kwa jina la Swalha, aliyekuwa akijishughulisha na masuala ya urembo (make up artist) ameuawa kwa kupigwa na risasi saba na mumewe usiku wa kumkia Jumapili ya jana May 29. Tukio hilo limetokea nyumbani kwa wanandoa hao huko Buswelu huku chanzo kikielezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Taarifa kutoka kwa watu wa karibu zinasema kuwa mume wa Swalha anayejulikana kwa jina la Said alichukua uamuzi huo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Amesema Swalha alienda kuangalia mpira mechi ya fainali ya Uefa kati ya Liverpool na Real Madrid
na akachelewa kurejea nyumbani.
Mumewe hakufurahishwa na kitendo cha mkewe kuchelewa kurudi nyumbani hivyo kukazuka ugomvi baina yao hali iliyopelekea mume wa Swalha kumfyatulia risasi.
Post a Comment