DIDIER GOMES ASHIKA NAFASI YA 4 YA KOCHA BORA AFRIKA
Siku kama ya leo Tarehe 10/10/2021 Alizaliwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Mfaransa Didier Gomes Da Rosa.
Kocha Didier Gomes aliingia Nchini Tanzania kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuwatumikia wekundu wa Msimbazi Simba SC Kama Kocha Mkuu na Kutamburishwa rasmi mnamo tarehe 24/01/2021 Mwaka Huu.
Gomes katika Historia yake mpaka sasa ameshatumikia takriban timu 10 akiwa kama Kocha Mkuu huku Simba SC ikiwa ni ya 11 kwake.
Timu Hizo ni;- AS Cagnes, Cannes B, Rayon Sports FC, Coton Sports FC, CS Cosntantine, JMS Skikda, Ethiopia Bunna, Horoya, Ismaily, Al-Merrikh na sasa yuko Simba SC.
Kama ulikuwa Hujui, katika Orodha ya Makocha bora Barani Afrika , Jarida la Ghana Sport Online linawataja makocha wawili ambao wanafundisha soka nchini Tanzania kama miongoni mwa makocha bora Afrika 2021 .
Kocha wa Mkuu wa Klabu ya Simba SC Didier Gomes Da Rosa anatajwa kama kocha Bora akishika nafasi ya 4 Afrika mwaka 2021, huku George Lwandamina wa Azam FC FC anatajwa kama ni kocha namba 10 kwa ubora
barani Afrika.
Orodha kamili;-
1. Pisto Mosmane ( Al Ahly)
2. Moeni Chaabani (Esperance)
3. Manqoba Mngqith (Mamelod)
4. Didier Gomes ( Simba SC)
5. Faouze Benzart ( Wydad Casablanca)
6. Nabil Kouki (Es Setif)
7. Ben McCarthy ( Amazulu FC)
8. Aboubacar Soulymonou ( Coton Sports )
9. Samuel Boudu ( Heart of Oak)
10. George Lwandamina ( Azam FC)
Vipi Wewe Kwa Upande Wako, Kocha Wako Anashika Namba Ngapi Hapo?
Post a Comment