BERNARD MORRISON ARUDI NA MOTO ATUPIA BAO
Winga Mghana wa Simba, Bernard Morrison ‘BM3’ amerudi na moto wake baada ya jana kufunga moja ya mabao yaliyoipa ushindi wa mabao 4-1 timu yake dhidi ya Cambiaso katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Bunju Veterani.
Morisson ataanza kuonekana katika kikosi cha Simba kwenye mechi ya Galaxy baada ya kutocheza mchezo wowote wa mashindano kutokana na kuwa kifungoni akitumikia adhabu.
Katika mchezo huo wa jana, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 yakiwekwa kimiani na beki Pascal Wawa kabla ya Morrison kuongeza la pili kwa friikiki nje ya 18, Abdulswamad Kassim alifunga la tatu na Hassan Dilunga kuhitimisha kapu la kufunga bao la nne.

Post a Comment