"Wananchi hawana matarajio mengine kwa serikali zaidi ya yale waliyotuchagua nayo ambayo tuliwaahidi wakati wa uchaguzi mkuu kupitia ilani ya CCM ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 hivyo ni lazima sisi tuliopewa dhamana tukaachana na urasimu na maslahi binafsi katika kutekeleza majukumu yetu"
"Napenda kuwakumbusha viongozi na watendaji kuwa dhamana walizonazo kwenye ofisi za umma ndani ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na CCM chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan wananchi wanahitaji maji, ajira, mazingira rafiki ya kibiashara, huduma bora za afya na heshima wanapofika kwenye ofisi za umma kupata huduma. Haya yakikosekana wananchi hawatatuelewa. Hivyo ni lazima sisi kama chama tutafuatilia na kuisimamia serikali ili kuhakikisha haya yanatekelezwa kwani tuliyaahidi na moja ya sifa kuu ya chama chetu ni kuahidi na kutekeleza"
"Hospitali hii ya kanda ya Mtwara mbali na kuwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 pia ni utekelezaji wa azimio la kikao cha halmashauri kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Mtwara mwaka 1987 lililotaka ujenzi huo kufanyika"
"Ujenzi wa hospital hii ya kanda Mtwara unagharimu takribani bilioni 15, kukamilika kwake kutawasaidia wananchi wa mikoa hii ya kusini ikiwemo Mtwara kuepuka kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za kibingwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na gharama za muda na fedha"
"Pamoja na kasi nzuri ya ujenzi inayofanywa na mkandarasi ambaye ni shirika la Nyumba la Taifa, wizara ya afya imekuwa kikwazo kikubwa katika kuhakikisha hospital hii inakamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi. Hawajamlipa mkandarasi hati za makipo takribani 4 ambazo ziliwasilishwa muda mrefu"
Aidha, Shaka ameitaka Wizara ya Afya kuacha sinema za maonesho kwa kutoa maelekezo na ahadi zisizotoa matokeo yanayopimika na kuonekana kwa wananchi.
0 Comments