Advertisement

Responsive Advertisement

KENANI; CCM HAITAVUMILIA UZEMBE, UBADHILIFU WA FEDHA

Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg Kenani Laban Kihongosi (MNEC) amesema Chama cha Mapinduzi hakito wafumbia macho watendaji wazembe wa Serikali na hakito fumbia macho uzembe na ubadhilifu wa fedha za Umaa.

Amezungumza hayo alipotembelea mradi wa hospitali ya Wilaya ambao alikuta Hakuna Vipimo vya Nondo, Mabomba yaliyotumika kukiuka taratibu za manunuzi ya serikali, pia mkataba wa ujenzi wa wodi tatu umeisha na majengo hayajakamilika, ameagiza uchunguzi ufanyike ili kujua kwanini kuna Mkwamo katika Mradi huo.

Akizungumza katika ziara yake ya Kikazi katika Wilaya ya Mtwara vijijini Katibu Mkuu Amesisitiza wajibu wa CCM ni kuisimamia Serikali iliyoiunda na kufikisha Maendeleo kwa wananchi kwa wakati ili wapate huduma iliyo Bora katika maeneo yao.

Kenani amesema Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kufanya Mapinduzi ya kiuchumi kwenye sekta mbalimbali katika kufikishia Maendeleo wananchi wa Chini katika maeneo wanayoyazunguka .

"Mimi Kama Kijana aliyeniamini katika kutumikia Taifa letu nipo tayari kuwasaidia wananchi nyie wa Mtwara vijijini katika kuhakikisha Maendeleo yanafika kwa wakati na huduma nyingi ziwafikie kwa wakati ili kuendelea kumuunga Mkono Rais wetu"

Hata hivyo Katibu Mkuu Kenani amesema Chama watakuwa wakali sana katika kuisimamia Serikali, kwani ni wajibu wa Chama kufanya hivyo na ndio maana hata wao wametoka juu kushuka chini na kukagua Ilani itekelezwe kama iliivyo ahidi.

"Kenani amepongeza na kusema amefurahishwa na Mradi wa tofali ambao halmashauri imeweza kuwawezesha 4% hivyo niwaombe halmashauri nyingine Nchi nzima kuhakikisha mnaendelea kutenga asilimia za Vijana ili Vijana waweze kufanya kazi kuendana na Kasi ya Mh.Rais Samia Suluhu Hassani"-Kenani.

Pia amepongeza ujenzi wa shule ya Dinyecha kwani imejengwa kwa ubora na thamani ya fedha inaonekana amesisitiza utunzwaji wa miundombinu ya shule ili idumu kwa vizazi vijavyo.

Aidha Kenani amewaomba wananchi wa Mtwara vijijini kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi kinavyofanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani yake kikamilifu.

Post a Comment

0 Comments