"Ilikuwa ndoto yangu, nilijinyima nikapoteza mpaka mashabiki lengo ilikuwa nikutimiza hili, nimeanza kujenga tangu mwaka 2018 niliponunua kiwanja, unajua Wasanii tunaishi maisha ya kufeki nilichoka kupanga, ramani nimechukua kwenye moja ya mjengo niliowahi kupanga”---- Amesema Nisha
“Wenye nyumba walionipangishaga wamekuja na wamefurahi kuniona na kwangu sasa, nimejenga kwa hela za movie lakini pia Nishas Wedding vilevile michezo ya kuweka hela na kukopa ya kina Mama imesaidia, kwa wengine hii inaweza kuwa ndogo lakini kwangu ni kubwa sana na nina mshukuru Mungu sana."---- Amesema Nisha
0 Comments