Advertisement

Responsive Advertisement

MWONEKANO WA DARAJA JIPYA LA WAMI

Muonekano wa nguzo za Daraja jipya la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 61 na unatarajia kukamilika mwezi Novemba, 2022.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amemtaka mkandarasi Power Construction Cooperation Ltd kutoka China anayejenga Daraja jipya la Wami kuongeza kasi ili kukamilisha ujenzi kabla ya muda walioongezewa kwenye mkataba kumalizika.

Prof. Mbarawa aliitoa agizo hilo wakati akikagua maendeleo ya daraja hilo lenye urefu wa mita 510, upana wa mita 11.85 lililoko mkoani Pwani.

Daraja hilo ni kiungo muhimu kutoka Mji wa Chalinze kwenda mikoa ya kaskazini mwa nchi na nchi za jirani.

Post a Comment

0 Comments