Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameweka mikakati madhubuti unayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vijiji vyote nchini vikiwemo vya wilaya ya Bukoba mkoni Kagera.
Amesema Serikali inaendelea kutekeleza kampeni ya Rais Mheshimiwa Samia ya kumtua mama ndoo kichwani ili kuhakikisha huduma hiyo inapatikana karibu na kuwawezesha wanawake na vijana katika maeneo mbalimbali nchini hususani ya vijijini kupata muda wa kushiriki katika shughuli za kijamii.
Mheshimiwa Majaliwa ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Septemba 21, 2021) wakati akizungumza na wananchi katika kata ya Kemondo baada ya kukagua ujenzi wa mradi wa maji wa Kemondo-Maruku akiwa katika katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika mkoa huo.
Waziri Mkuu amesema Serikali imeweka mikakati madhubuti yenye lengo la kumaliza tatizo la maji nchini, hivyo wananchi waendelee kuwa na subra kwani mradi huo utakamilika kwa wakati na kwa viwango ili wapate huduma hiyo kama ilivyokusudiwa.
0 Comments