MWAYOMBO; YANGA BADO INAJIPANGA
Na Emmanuel Mwayombo JR.✍
Yanga ni timu ambayo bado inajijenga kwa sasa hivyo mashabiki wake kuamini timu hii inaweza kufanya makubwa katika michuano ya Kimataifa ni makosa makubwa .
Yanga msimu huu wamefanya usajili mzuri sana ambao kama mwalimu wao akiweza kuunganisha umoja ndani ya kikosi chao na muunganiko ukakubali basi Yanga itakuwa moja timu tishio katika ukanda wa Africa Mashariki.
Kitu kinachoirudisha nyuma Yanga ni kutamani kupata mafanikio kama ambayo wapinzani wao (Simba) wameyapata siku za karibuni. Wakati wanafikiria kufanikiwa mapema wanasahau wapinzani wao ile timu yao waliiunda kwa muda mrefu na walikuwa hawabomoi kikosi cha kwanza kila mwanzo wa msimu kama ambavyo Yanga wanafanya.
Siku zote huwezi kupata kikosi chenye muunganiko bora kama kila siku utabadilisha makocha na pia kusajili wachezaji wengi kila mara ambao utawaleta moja kwa moja kikosi cha kwanza na ukataka Matokeo kwao bila kuwapa muda wa kutosha ili wachezaji waweze kuelewana vilivyo kama ambavyo Simba kikosi Chao kimekaa kwa muda mrefu licha ya kuwa wanafanya maboresho baadhi ya maeneo.
Angalia safu ya ulinzi ya Simba ukitoa Onyango ambaye amekuja msimu ulopita wengine wote ni wachezaji ambao wako pamoja kwa zaidi ya misimu miwili hivyo muunganiko wao ulisha kubali muda mrefu sana hivyo viongozi wa Yanga wanatakiwa kutulia na kumwachia mwalimu kazi ya kusuka timu yao na mashabiki wawe wavumilivu kwani matokeo yatakuja tu baada ya timu yao kuwa sawa.
Kukipa majukumu makubwa kikosi hiki msimu huu ilikuwa ni kukionea Yanga, walitakiwa kusubiri hadi msimu ujao hapo sasa wangeweza kuwa na ndoto ya kufanya vema kwani hadi wakati huo timu yao itakuwa katika muunganiko wa hatari baada ya nyota wao Bangala, Djuma, Moloko, Aucho, Mayele, Makambo na wengine wote kuwa wameshasomana na kila mmoja anajua atacheza vipi na mwenzake.
Yanga sio timu ya kwanza kufanya vibaya hata wapinzani wao Simba walikaa miaka mitano wakiwa na maumivu na baadaye waligundua kosa lao wakajipanga na sasa wanafurahia matunda yao. Yanga kwa sasa inatakiwa kuunda kikosi ambacho kitakaa kwa muda mrefu hii ndiyo dawa ya kuwarejesha katika ushindani bila kufanya hivi kila msimu itakuwa inajijenga bila mafanikio.

Post a Comment