Advertisement

Responsive Advertisement

MBARONI KWA KUMCHEZEA MTOTO WAKE SEHEMU ZA SIRI

Jeshi la polisi mkoani Pwani linamshikilia,  Anthony Lugendo mkazi wa Mlandizi mkoani  humo kwa tuhuma za kumdhalilisha mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu.

Akizungumza na Binago Blog jana Ijumaa Septemba 17, 2021 mjini Kibaha Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amesema tukio hilo limetokea Jumatano katika kitongoji cha Kaloleni kata ya Janga mkoani  humo.

"Tulipata taarifa hiyo kutoka kwa raia wema  tukafanya haraka kwenda eneo  la tukio na tukamkuta mkazi huyo  akiendelea na unyanyasaji huo tukamamata, " amesema.

Amebainisha kuwa walimkuta mtuhumiwa huyo akiwa chumbani kwake amemvua nguo zote mtoto huyo anayesoma shule ya awali.

Ameeleza kuwa hivi  sasa wanamshikilia mkazi huyo  wakiendelea na hatua mbalimbali kabla ya kumfikisha mahakamani.

Katika hatua nyingine Wankyo amesema wamekusanya Sh119,130,000 za faini 3, 971 za makosa ya usalama barabarani.

& MR. PM.✍

Post a Comment

0 Comments