MAJALIWA ARIDHISHWA NA HATUA YA UJENZI WA RELI YA SGR
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa kassim Majaliwa amekagua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Dar es Salaam hadi Kilosa, Mkoani Morogoro na kusema kwamba ameridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa.
“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kukamilisha ujenzi wa miradi yote iliyoanzishwa, hivyo Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali yao, na tunawahakikishia mradi huu utakamilika kwa wakati.”
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo Jumapili, Septemba 12, 2021 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi ya mradi huo katika kituo cha Kwala kilichopo mkoani Pwani, ambacho kitatumika kama kituo kikuu cha kufanya matengenezo makubwa ya mabehewa na injini za treni.
“Maendeleo ya ujenzi huu yanatia matumaini na kazi inaendelea kwa ufanisi na eneo lililobaki la Pugu Dar es Salaam tunaamini litakamilika kwa wakati, nimeridhishwa na vituo vya abiria vilivyokamilika.”
Aidha, Waziri Mkuu amewasihi wafanyakazi wa mradi huo kufanya kazi kwa ufanisi kwani lengo la Serikali ni kuufikisha mradi huo katika mikoa ya Mwanza, Kigoma, Katavi katika bandari ya Karema.
“Njia zote za reli tunataka ziwe za kisasa, hii pia itawezesha kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, nchi yetu ni ya kimkakati kwa sababu nchi zote za jirani zinategemea reli hii”

Post a Comment