BASHUNGWA AKUTANA NA LUTENI JENERALI MATHEW MKINGULE
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa amekutana na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania Luteni Jenerali Mathew Mkingule na kufanya mazungumzo juu ya kuboresha ushirikiano baina ya wizara yake na Jeshi kwenye masuala mbalimbali ya michezo ikiwemo wataalamu, miundombinu ya michezo, usafiri, kuibua na kuendeleza vipaji kupitia vijana wanaojitolea kwa mujibu wa sheria katika Jeshi la kujenga Taifa JKT.
Katika kikao hicho kilichofanyika Agosti 31, 2021 jijini Dodoma, Waziri Bashungwa amemweleza Mnadhimu huyo nia ya Wizara ya Habari kushilikiana na jeshi hilo katika kuinua sekta ya michezo kwa kuwashirikisha wataalamu mbalimbali wa michezo ambao wapo katika majeshi mbalimbali hapa nchini ili waweze kuibua na kuendeleza vipaji vya wanamichezo nchini.
Waziri Bashungwa amesema Wizara yake imeona ni vyema kuwa na michezo ya kikamkati (Kipaumbele) ambayo ni ngumi na riadha kutokana na historia ya baadhi ya watanzania waliowahi kufanya vyema katika michezo hiyo na kung’ara kimataifa.
“Tunaamini kwa kushirikiana na jeshi, timu za Taifa zitaweza kufanya kambi katika maeneo ya jeshi, hii itaongeza nidhamu na ukakamavu wa timu zetu” Amesem Waziri Bashungwa.
Kwa upande wake Luteni Jenerali Mathew Mkingule amesema mazungumzo hayo ni hatua nzuri katika kukuza sekta ya michezo amesema taarifa ya mazungumzo hayo kwa Mkuu wa Majeshi kwa ajili ya kutolewa uamuzi.
Aidha, viongozi hao kwa pamoja wamekubaliana viongozi wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) kukutana na viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili kujadiliana namna bora na sehemu za kipaumbele za kushirikiana.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo amesema hatua ya majeshi kushiriki kwenye michezo mbalimbali hapa nchini ni fahari kwa nchi na itaisaidia kuiwezesha Tanzania kuibuka vinara katika michezo mbalimbali.

Post a Comment