Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 18/09/2021

*✨✨KESHA LA ASUBUHI, LESONI NA USOMAJI WA BIBLIA KWA MPANGO.  Jumamosi 18/09/2021.*

 *🌄#Kesha la Asubuhi:* 
 KAMWE USIMDHARAU MKOSAJI.
 _“Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema;.."  (Mathayo 12:35)_
🌅Kamwe usiwachukulie wale unaofanya nao kazi kuwa ni waaminifu isipokuwa una ushahidi dhahiri kwamba wao ni waaminifu. Na hata pale ambapo kukosa uaminifu kwa mfanyakazi kumethibitishwa wazi, hupaswi kushughulika naye Kwa namna ambayo itampa udhuru wa kusema "ulikuwa mkali". Hupaswi kufanya chochote ambacho kitamsababisha mkosaji kukasirika. Usihusiane na waumini au wasioamini Kwa namna ambayo itaamsha hisia mbaya kabisa za moyo. Usitoe shutuma ambazo zinaweza kuwa si za haki Kwa namna ya kikatili. Kwa mwelekeo kama huo unaweza kusababisha roho kuangamia kabisa.....

🌄Katika kazi yako unapaswa kudhihirisha huruma ya Kristo. Maneno yako yanapaswa kuwa udhihirisho wa huruma Yake. Unapaswa kuzungumza lugha ya Kanaani. Wewe si wa ulimwengu tena Umetoka ulimwenguni, na unapaswa kujitenga na njia na mazoea yake. Kwa maneno na matendo unapaswa kudhihirisha makusudi ya Mungu ya upendo. Daima unastahili kuwatendea wafanyakazi wenzako Kwa heshima.... 

🌅Yeye anayetumika badala ya Kristo, anatenda wajibu wake pale tu anapodhihirisha neema za roho wa Mungu kwa wale wanaohusiana naye. Hakupaswi kusikika neno lolote la kukaripia au la hasira, kwa sababu maneno kama hayo humwaibisha Kristo na kufedhehesha jina la Mkristo. Ni sehemu ya wajibu wa yule aliye katika utumishi kama kiongozi kujifunza jinsi ya kuheshimu. 
Bwana Yesu amewachagua wanadamu kuwa vyombo vyake. Wanapaswa kutekeleza makusudi yake. Kifo chake msalabani Kalvari kilikuwa ni kilele cha aibu Yake. Kazi yake kama Mkombozi iko nje ya dhana zenye kikomo.  Ni wale tu ambao wameifia nafsi zao, ambao maisha yao yamefichwa pamoja na Kristo katika Mungu, ndio wataweza kuwa na dhana ya ukamilifu wa sadaka iliyotolewa Kwa ajili ya kuokoa jamii iliyoanguka. 

🌅 _Katika maisha ya Kila siku tunapaswa kufuata mfano wa Kristo. Ndipo_ _katika maisha ya kidini itakuja imani ipitayo ufahamu._ Hatupaswi kujishughulisha na kazi yoyote au biashara ili kupata sifa heshima ya watu. Hatupaswi kusema neno hata moja au kufanya tendo hata moja ambalo litapunguza katika akili za wengine sifa nzuri waliyonayo ya Yule aliyekufa kifo cha aibu msalabani ili apate fursa ya kuwaokoa adui zake.
 *- Letter 196, Septemba  18, 1901., to an administrator at the St. Hellen Sanitarium.*


#LESONI: PUMZIKO LA MWISHO.
 *Fungu la kukariri:* _“lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio_ _halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo_ Mungu aliwaandalia wampendao.
 (1 Wakorintho 2:9)_ 

✍️ Je, umewahi kuhisi kuwa ulikuwa katikati ya pambano kuu, namna ya pambano kati ya wema na uovu? Wengi, hata watu wa kidunia wamehisi uhalisia huu. Na tutahisi hivyo Kwa sababu, naam, ni kweli. Tupo katika pambano kuu kati ya wema na uovu, kati ya Kristo (wema) na shetani (ubaya). Maisha basi, yanatumiwa katika viwango viwili. Pambano kuu kati ya Kristo na shetani linaendelea duniani pote, Kwa kweli, hata kiwango cha kiulimwengu, Kwa kuwa mbinguni ndipo lilipoanzia kwanza (Ufunuo 12:7). Bali, katika machafuko ya matukio, tunaweza kupoteza mtazamo mpana wa mpango wa Mungu kuokoka kwa ulimwengu huu. *Vita, machafuko ya kisiasa, majanga ya asili yanaweza kutushikilia katika* *hofu pasipo msaada. Lakini uongozi wa Mungu wa kiunabii unaweza kutusaidia* *kudumisha taswira pana ya tunakokwenda na tutakavyofika huko.* 

✍️✍️ _Pambano kuu linapiganwa zaidi sana katika kiwango cha mtu binafsi. Sisi_ _sote mmoja mmoja tunakabiliwa na changamoto ya imani katika maisha yetu ya_ _kila siku, na ikiwa hatutaishi hata wakati wa kuja Yesu mara ya pili, tutakabili kifo, pia._ Juma hili tunaangalia namna tunavyoweza kupumzika ndani ya Yesu katikati ya machafuko pote duniani na wakati wetu ujao binafsi usiojulikana, angalau kwa kipindi kifupi. Katika kipindi kirefu, mambo yanatia matumaini mema, kwa kweli!


#BIBLIA KWA MPANGO.
 *1 Wakorintho 9* 
¹ Je! Mimi si huru? Mimi si mtume? Mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Ninyi si kazi yangu katika Bwana?
² Kwa maana ikiwa mimi si mtume kwa wengine, lakini ni mtume kwenu ninyi; kwa maana ninyi ndinyi muhuri ya utume wangu katika Bwana.
³ Hilo ndilo jawabu langu kwa wale wanaoniuliza.
⁴ Je! Hatuna uwezo wa kula na kunywa?
⁵ Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?
⁶ Au je! Ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo wa kutokufanya kazi?
⁷ Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi?
⁸ Je! Ninanena hayo kwa kibinadamu? Au torati nayo haisemi yayo hayo?
⁹ Kwa maana katika torati ya Musa imeandikwa, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Je! Hapo Mungu aangalia mambo ya ng'ombe?
¹⁰ Au yamkini anena hayo kwa ajili yetu? Naam, yaliandikwa kwa ajili yetu; kwa kuwa alimaye nafaka ni haki yake kulima kwa matumaini, naye apuraye nafaka ni haki yake kutumaini kupata sehemu yake.
¹¹ Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini?
¹² Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo.
¹³ Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu?
¹⁴ Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.
¹⁵ Lakini mimi sikutumia mambo hayo hata moja. Wala siyaandiki hayo ili iwe hivyo kwangu mimi; maana ni heri nife kuliko mtu awaye yote abatilishe huku kujisifu kwangu.
¹⁶ Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili!
¹⁷ Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili.
¹⁸ Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili.
¹⁹ Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi.
²⁰ Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria.
²¹ Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria.
²² Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.
²³ Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine.
²⁴ Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate.
²⁵ Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.
²⁶ Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;
²⁷ bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.

✍️ *TAFADHALI, SHIRIKI HABARI HIZI NA WENGINE. BWANA AKUBARIKI SANA🙏🙏.*

Post a Comment

0 Comments