UMMY AWATAKA WA CEO KURIPOTI MAPEMA MAKAO MAKUU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu anawatangazia Wakurugenzi wote wapya 69 walioteuliwa kwa mara ya kwanza, kuripoti Makao Makuu ya Ofisi za Rais -TAMISEMI - Dodoma tarehe 05.08.2021 kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma - Mkapa House
kuanzia saa 3.00 asubuhi kwa ajili ya kupatiwa maelekezo mbalimbali.
Wakurugenzi hao wanatakiwa kuripoti wakiwa na Cheti cha kuzaliwa, Kitambulisho cha NIDA, Wasifu Binafsi (Cu), Vyeti vya Kitaaluma pamoja na picha mbili (Passport Size).
Wakurugenzi ambao wamehamishwa vituo na wale walioendelea kuwepo kwenye vituo vyao vya awali waendelee na utaratibu wa kwenda kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi kwa ajili ya makabidhiano kuanzia tarehe 03.08.2021.
Halkadhalika Wakurugenzi ambao uteuzi wao umesitishwa wakaripoti kwa Makatibu
Tawala wa Mikoa yao mara moja.
Post a Comment