Advertisement

Responsive Advertisement

TWITTER WAMFUNGIA AKAUNTI KIONGOZI WA UPINZANI INDIA

Twitter imeifungia akaunti ya kiongozi mkuu wa chama cha upinzani nchini India Rahul Gandhi, baada ya kutupia picha yake na wazazi wa msichana wa miaka tisa wa Dalit ambaye anadaiwa kubakwa, kuuawa na kuchomwa moto na kasisi wa Kihindu.

Uchapishaji wa picha hiyo umetajwa kukiuka sheria za faragha za Twitter.

Chombo cha haki za watoto cha India kiliomba Twitter kuondoa picha hiyo, ikisema kwamba iliruhusu utambulisho wa mwathiriwa wa ubakaji kufunuliwa, ambayo ni marufuku chini ya sheria ya India.

Gandhi jana Ijumaa alisema kuwa kwa kufunga akaunti yake ya Twitter ni mpango wa kuingilia mchakato wa kisiasa wa India na kuwanyima wafuasi wake zaidi ya milioni 19 haki yakutoa  maoni.

Post a Comment

0 Comments