Advertisement

Responsive Advertisement

DUNIA KUWA UWANDA WA DURA SIKU ZA USONI SIO MBALI

#DUNIA KUWA #UWANDA WA #DURA SIKU ZA USONI NA SIYO MBALI.

DANIELI 3:1
Nebukadreza mfalme alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini na upana wake dhiraa sita, akaisimamisha katika uwanda wa #dura, katika wilaya ya babeli.

Rafiki zangu wasomaji na wasafiri wenzangu! BWANA YESU asifiwe mno🙏🏻, nawakaribisha tena katika somo tajwa hapo juu.

Ukitaka kulielewa hili somo mpendwa rafiki, soma sura yote ya danieli 3:1 - 30

Babeli ulikuwa ni utawala wenye nguvu duniani na ambao sifa zake zilifika kila pande ya dunia ya wakati huo. Ufalme tajiri na wenye fahari, uliokuwa ukiongozwa na mfalme #NEBUKADREZA.

 Huyu mfalme wakati wa flani aliota ndoto ya ajabu ya sanamu kubwa iliyokuwa ikielezea falme zitakazofuata kutawala dunia baada ya ufalme wa babeli kuanguka.

Lakini baada ya ndoto hiyo mfalme huyu Nebukadreza aliamua kusubu sanamu kubwa mno ya dhahabu na kuisimamisha katika uwanda wa #Dura pale babeli. Siku ya uzinduzi wa hiyo sanamu ya miungu yake ilifika.

Taarifa zilipelekwa kila mahali ambapo utawala wa babeli ulienea. Viongozi wote waliokuwa katika serikali waliitwa kuhudhuria hiyo ibada ya sanamu. Na hawa wte walisimama mbele ya hiyo sanamu

Tangazo lilitolewa likisema, kila kabila, taifa, na lugha zote , mtakaposikia hivi vyombo vyote vya mziki, filimbi, zeze, santuri, kinubi, zomari na ngoma aina zote, Lazima kuanguka na kuisujudia sanamu ya dhahabu aliyoisimamisha mfalme nebukadreza. Yeyote asiyeisujudia hiyo sanamu lazima atauawa.

Katika tukio hilo walikuwepo vijana watatu kutoka Yuda tena walikuwa ni mateka katika hiyo nchi ya babeli. Ngoma zilipopigwa na filimbi na zeze na santuri na zomari pia kinubi, BIBLIA inasema, watu wote na mataifa na lugha waliisujudia ile sanamu ya miungu ya mfalme. Lakini wale vijana watatu hawakuisujudia ile sanamu ya dhahabu ya mfalme nebukadreza.

Napenda nikuambie ndugu msomaji, YESU anakuja kuchukua watu wake wenye msimamo katika ibada ya kweli ya MUNGU Muumbaji . Watu ambao hawatayumbishwa na vitisho vya watawala wa dunia hii. Watu ambao watajibu bila woga kuwa sisi hatuko tayari kuisujudia sanamu ya mnyama, wala hatuko tayari kushusha viwango vyetu vya imani ili kufanana na ninyi, watu walio tayari kusema, MUNGU wetu tunayemtumikia atatuokoa na hata kama hatatuokoa leo, hatuko tayari kuisujudia sanamu ya mnyama.

Pambano kuu lilitangazwa katika utawala wa babeli na liliwalenga washika amri kumi za MUNGU ikiwemo na sabato. Siku zote shetani anawawinda wale wanaozishika AMRI za MUNGU na imani ya YESU . Shetani hana shida na wajiitao wakristo lakini hawazishiki amri za KRISTO . Anajuwa kuwa hao ni mali yake na siyo watu hatari katika ufalme wake . Watu hatari katika ufalme wa Shetani ni watunza sabato ambao wanazishika amri kumi za MUNGU , watu waaminifu.

Danieli mtunza AMRI kumi za MUNGU , mtu mwaminifu mno kule babeli, pia alipitia pambano lililomlenga ili kumuangamiza asiwepo ili mamlaka ya shetani isipingwe.

Danieli 6:1-28
Watu waovu walimwonea kijicho danieli katika ikulu ya mfalme dario ktk utawala wa waajemi na wakiongozwa na shetani walitafuta sababu ya kumshitaki ili auawe. MUNGU alimlinda Nabii katika saa ya hatari na alimuokoa katika tundu la simba wenye njaa.

Rafiki msomaji, je wajuwa kuwa mda si mrefu dunia itakuwa kama uwanda wa #Dura? Adhabu na mauaji yataamuriwa dhidi ya wale wanaokataa kuitii mamlaka yaupapa itakaposhika hatamu kuongoza dunia na serikali zote pamoja na dini zote???

Nataka nikuambie jibu ni ndiyo. Saa ipo mbele nayo yaja kwa haraka sana.

Ufunuo 13:1-18

Katika kitabu cha ufunuo tunaziona mamlaka kubwa mbili, moja iliyo na pembe mbili mfano wa mwanakondoo  (Hili ni Taifa kubwa lenye nguvu duniani) ambalo linatumika kwa ile mamlaka ya kwanza ambayo jeraha lake la mauti lilipona(hii ni roma ya kidini).

Unabii unasema kuwa watu watalazimishwa kuusujudia upapa na ambaye atakataa atauawa. Kumsujudia papa ni kumsujudia shetani .  Ufunuo 13:2👉🏻 na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule Joka(shetani) akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.

Yohana anauona huu ufalme wa kidini katika sura za wanyama watatu, chui, dubu na simba.

Chui aliwakilisha utawala wa wayunani ambao walipenda sana kuabudiwa na kusujudiwa lakini pia walikuwa ni katili mno.

Dubu aliwakilisha wamedi na waajemi ambao pia walikuwa ni wakatili mno lakini pia walipenda kusujudiwa na Wanadamu wenzao.(rejea danieli 6:1-28)

Simba aliwakilisha utawala wa babeli wenye nguvu na uwezo mwingi, watawala wake walipenda kusujudiwa na kusujudia sanamu, pia walikuwa ni wakatili.

Sasa mnyama huyu ambaye yohana anamuona anazo tabia hizi. Toka taasisi ya upapa ianzishwe, Papa wanapenda sana kupigiwa magoti/kusujudiwa, lakini pia wana tabia ya ukatili sana na hawana huruma ndani ya mioyo yao kama walivyo wale wanyama chui, dubu na simba. Historia inasema huko nyuma miaka elfu na zaidi iliyopita, wakati mapapa wa roma wakitawala dunia, serikali na dini zikiwa chini yao, mauaji makubwa yalifanyika chini ya mamlaka hii ya kidini kwa watu wote ambao waliipinga, walifyekelewa mbali na makaburi ya watu hawa yaliandikwa maneno ya kukatisha tamaa "#kifonichaMilele"

Kwahiyo unabii uko sahihi. Alilolisema MUNGU litatimia na mda siyo mrefu mtaliona ikiwa tutakuwa hai.

WAADVENTISTA Wasabato wengi mnapaswa kujiandaa tangu sasa. Na huko mbele tuendako naamini tutagawanyika, wapo watakaosema kama shadrak ,meshack na abednego na wapo watakaosema kama mke wa Ayubu.

Wengi wetu makanisani wamejenga imani yao kwa wachungaji wanaowahubiri injili lainilaini na kuwatazamisha kwenye mafanikio ya dunia hii na maendeleo ya miaka elfu, watu wa hivi watafagiliwa mbali kabisa. WASABATO Jina watafyekelewa mbali watatupwa kama takataka za mavi.

Huu ni wakati wa kufanya mapatano na MUNGU wetu, kumrejea BWANA kwa unyenyekevu, na siyo wakati wa kuwafunga midomo watumishi wa MUNGU wenye ujumbe. Yapo makanisa yamewafunga midomo #Wajumbe wenye #Ujumbe. Na sasa wanajilisha makapi wakudhani ndiyo ujumbe. Shetani anao mawakala hadi humu makanisani, wengine ni wachungaji , wengine ni wainjilisti, wengine ni makatibu, wengine ni wahazini, wengine ni wanakwaya, wengine ni wachambuzi wazuri wa lesoni na wengine ni washiriki . Amewaweka hapo ili ujumbe wa malaika watatu usihubiriwe.

Tunakaribia kwenye pambano kuu la mwisho. Litakuwa ni kali na la kutisha, lakini la mda mfupi. YESU atasimama wakati huo ili kupigana upande wa watu wake waaminifu.

Dunia itakuwa ni #UWANDA WA #DURA.

YESU anakuja kuchukua watu wenye msimamo, siyo watu wanaoyumbayumba katika imani hao ni makapi na moshi tu.

Leo Danieli , shadrack, Meshack na Abednego wangekuwepo ndani ya Sda, hakika washiriki wengi wangewapinga hawa ndugu . Tena wangeitwa majina ya ajabu, kama wenye itikadi kali, waasi hawa, wazushi na yumkini wangeitwa #warifoma.

👉🏻Yaani tuna wakati mgumu huko tuendako. 

BWANA MUNGU atusaidie tu. Yordani inazidi kufurika, ni nani atatuvusha?? Ni YESU peke yake atakayetuvusha ikiwa tutaachana na mambo ya dunia. Usipoachana na mambo ya dunia hii, hakika kwenye pambano kuu wakati wa taabu kuu, hutovuka, utaanguka, utakuwa msaliti mkubwa wa ndugu zako.

BWANA YESU anakuja.
Ubarikiwe mno kwa kusambaza ujumbe huu.

Mimi mjoli mwenzako: Pambano IBR CH.

Post a Comment

0 Comments