Advertisement

Responsive Advertisement

TRA WATOA POLE, WATUMISHI 5 WALIOFARIKI KWENYE AJALI

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa majonzi na masikitiko makubwa imetoa taarifa ya vifo vya maofisa watano waliokuwa watumishi katika Idara ya Ushuru na Forodha vilivyotokana na ajali mbaya ya gari alfajiri ya tarehe 23 Agosti, 2021 eneo la Hanseketwa, Old Vwawa Wilaya ya Mbozi katika mkoa wa Songwe, Maofisa waliofariki ni;- Bw. Benard Balagi Mushingi (40) Afisa Forodha (TRA-Songwe), Bw. Azaria Asakwe Sivonike (42) Dereva (TRA-Mbeya), Bw. Joel Isaya Mitondwa (36) Afisa Forodha (TRA-Mbeya), Bw. Said Mrisho Buddy (34) Afisa Forodha (TRA- Mbeya), Bw. Fahad Hassan Haji (26) Afisa Forodha Msaidizi (TRA- Mbeya).

"TRA inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na watumishi wa TRA kwa kuondokewa na wapendwa wetu ambao walikuwa siyo tu nguzo muhimu katika Mamlaka ya Mapato bali pia Taifa kwa ujumla"

Aidha, TRA imesema Familia ya TRA itaendelea kuwakumbuka marehemu wote watano na kuenzi mchango wao katika kazi ya kukusanya mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo ya taifa,"-----> Sisi watumishi wenzao, vifo hivi vimetuacha na simanzi kubwa na pengo lisilozibika kirahisi kwa nguvu kazi tuliyoipoteza pamoja na kuzingatia maarifa na weledi waliokuwa nao"

"Mwenyezi Mungu awape marehemu wote pumziko la amani na tunaombea familia zao Mungu aweze kuwapa nguvu za kuhimili mshtuko na pigo kubwa lililotokana na vifo hivi kwa vijana wetu, Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. Wapumzike kwa Amani. Amina."---- TRA

Post a Comment

0 Comments